Maukibu ya Ataba mbili imeomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Maukibu ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Majlisi imeshuhudia ushiriki wa mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami na kundi kubwa la watumishi wa Ataba mbili tukufu.

Maukibu imefanya matembezi yake kuandia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, ikaenda hadi malalo ya Imamu Hussein (a.s) kumpa pole kutokana na msiba huo, katika matembezi hayo waombolezaji wameimba qaswida na tenzi za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi.

Uombolezaji umehusisha ubebaji wa jeneza la Imamu Alkadhim (a.s) la kuigiza, ili kutengeneza mazingira ya huzuni zaidi.

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu huomboleza kumbukizi za vifo vya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka kupitia maukibu ya pamoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: