Mazuwaru wanahuisha usiku wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Rajabu ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Zuwaru waliokuja katika mji wa Karbala, wamehuisha usiku wa Ijumaa ya mwisho katika mwezi wa Rajabu Aswabu mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mji umeshuhudia idadi kubwa ya zuwaru waliokuja kuhuisha usiku huu, sambamba na kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s), zuwaru huhuisha usiku huu kwa kufanya ziara na kusoma dua.

Mji wa Karbala hupokea watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo mbili takatifu na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa utaratibu maalum wa kukidhi mahitaji ya zuwaru na kutoa huduma bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: