Ibada ya kusoma Dua hiyo tukufu imefanywa katika mazingira tulivu, kwa ushiriki wa idadi kubwa ya zuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, huweka mazingira mazuri ya usomaji wa dua hiyo kila wiki, huandaa vitabu vya dua, sehemu maalum ya kufanyia ibada, kupuliza marashi pamoja na huduma zingine.




