Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unafanya shindano la kitamaduni katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majina ya washindi yatatangazwa siku ya Ijumaa 23/01/2026m sawa na mwezi tatu Shabani kupitia majukwaa ya Atabatu Abbasiyya.
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa ahudhurie katika hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwezi wa bani Hashim (a.s), itakayofanywa katika uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumamosi tarehe 4 Shabani 1447h, sawa na tarehe 24/01/2026m saa 12:30 jioni baada ya swala ya Magharibi na Ishaa.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria kwenye hafla, atatakiwa kwenda katika ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi wiki mbili kuandia kutolewa kwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria) kwa ajili ya kupokea zawadi yake.
