Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha siku ya Qur’ani kitaifa

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha siku ya Qur’ani kitaifa.

Usomaji wa Qur’ani umefanywa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya ujumbe kutoka kituo cha Qur’ani katika taasisi ya Mustwafa (s.a.w.w) na kundi kubwa la zuwaru.

Mjube wa kamati ya maadhimisho katika Ataba tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema “Hafla inaendana na kumbukumbu ya kupewa utume kwa Mtume (s.a.w.w) na siku ya kimataifa ya Qur’ani, wameshiriki wasomaji wa Ataba tukufu ili kushajihisha utamaduni wa kusoma Qur’ani”.

Hafla imeshuhudia usomaji wa Qur’ani kutoka kwa msomaji wa Atabatu Alawiyya Karim Mansuri, msomaji wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya Osama Karbalai na Muhammad Ridhwa Zubaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: