Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) imekamilisha maandalizi ya kongamano la Ghaithu-Samaa awamu ya pili

Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha maandalizi ya kongamano la Ghaithu-Samaa la mwaka wa pili.

Kongamano litafanywa ndani ya ukumbi wa kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s) siku ya ishirini na nane katika mwezi wa Rajabu, sawa na tarehe 18/01/2026m, chini ya kauli mbiu isemayo (Baina ya uaminishu wa Khadija na mwanzo wa rehema kwa walimwengu), sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kupewa Utume kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na siku ya Qur’ani kitaifa.

Maandalizi yamehusisha uandaaji wa ukumbi na kuwema mahitaji ya lazima yatakayofanikisha shughuli za kongamano, pamoja na kuandaa zawadi za kutabaruku watakazopewa watafiti na washiriki wa kongamano.

Kongamano hilo ni sehemu ya juhudi za vitengo vya Atabatu Abbasiyya ya kufanikisha tukio hilo adhim la Qur’ani na utamaduni katika muonekano unaoendana na utukufu wake na misingi ya kibinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: