Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imegawa zawadi kwa washiriki wa kongamano la Ghaithu-Samaa awamu ya pili.
Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani, chini ya ofisi hiyo, imefanya kongamano lenye kauli mbiu isemayo (Baina ya uaminifu wa Khadija na kuanza rehema kwa walimwengu), sambamba na maadhimisho ya kumbukizi ya kupewa Utume na maadhimisho ya siku ya Qur’ani kitaifa.
Utoaji wa zawadi umehusha vipengele vya usomaji wa Qur’ani, kikiwemo kikosi cha (Sinal-Huda), kama sehemu ya kuonyesha kujali juhudi zao katika kufanikisha ratiba ya kongamano.
Utoaji zawadi huo ni sehemu ya harakati za idara ya Fatuma binti Asadi (a.s), katika kuwatia moyo wanawake na kuimarisha kiwango cha ushiriki katika harakati za kitamaduni na Qur’ani pamoja na kuimarisha nafasi ya mwanamke katika jamii.
Kongamano ni moja ya majukwaa ya Qur’ani ya wanawake, ambalo linaimarisha ushiriki wa wanawake na kujenga mazingira mazuri yanayoendana na mtazamo wa Ataba katika kutumikia Qur’ani tukufu.



