Shekhe Muhammad Nabahani kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa amesema: “Maahadi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha siku ya Qur’ani kitaifa sambamba na siku ya kupewa utume, imehusisha idadi kadhaa ya wasomaji wa Qur’ani”.
Akaongeza kuwa “Katika hafla hiyo yametolewa mawaidha kuhusu umuhimu wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukifanyia kazi, wamehimizwa wazazi kuwafundisha watoto wao usomaji wa Qur’ani na kuwaingiza katika semina za Qur’ani zinazofanywa na Maahadi, ili kuwalinda na vita vya kitamaduni inayowalenga”.
Majmaa-Ilmi kupitia harakati zake mbalimbali, hulenga kueneza utamaduni wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu katika jamii.






