Marjaa-Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, ametuma salam za rambirambi kufuatia kifo cha Allamah Sayyid Ali Salmani katika mji wa Ihsaa.
Muheshimiwa Marjaa mkuu katika salam za rambirambi amesema:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Allamah Hujjatu Islami walmuslimina Sayyid Ali Sayyid Naasir Salmani (r.a), umri wake mtukufu ameutumia katika kutetea sharia na kusimamia waumini, Mwenyezi Mungu ampe malipo mema.
Natoa mkono wa pole kwa familia yake tukufu na hauza takatifu katika mji wa Ihsaa na waumini wote kwa ujumla, kutokana na msiba huu mkubwa, namuomba Mwenyezi Mungu amfufue pamoja na babu zake watakatifu na ampandishe daraja, aidha aipe familia yake na wapenzi wake wote subira na uvumilivu.
Hakuna hila wala mguvu ispoluwa kwa Mwenyezi Mungu mkuu.
29/ Rajabu/ 1447h.

