Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameweka maua, mapambo na mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), milangoni na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, kama sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.
Atabatu Abbasiyya imetangaza mkakati maalum wa kuadhimisha kumbukizi hiyo, unaohusisha shughuli za kidini na kitamaduni, zitakazofanywa katika maeneo tofauti yaliyochini ya Ataba tukufu.
Atabatu Abbasiyya huweka muonekano wa furaha katika kuadhimisha kumbukizi za kuzaliwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), wakiwemo watakatifu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.














