Kufuatia kuingia mwezi wa Shabani.. Atabatu Abbasiyya imeweka mapambo kwenye dirisha la malalo ya Abuladhil Abbasi (a.s)

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameweka shada za maua juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Shabani.

Watumishi wa idara mbili, idara ya kusimamia haram takatifu na idara ya Masayyid, wameweka shada za maua juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Shabani na kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa wajukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Harakati hiyo ni sehemu ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika mwezi mtukufu wa Shabani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: