Kamati kuu ya kuhuisha turathi imechapisha toleo la pili la jarida la Ihyaa

Kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya, imetoa chapisho la pili la jarida la Ihyaa.

Nalo linachukua nafasi ya jarida la kituo cha Shekhe Tusi la utafiti na uhakiki chini ya kamati.

Toleo limesheheni risala mbalimbali za elimu muhimu, miongoni mwake ni:

Risala ya Sayyid Muhammad Haadi Almilani katika swala la uogaji wa janaba, Risala ya Shekhe Muhammad Baaqir Alfashariki katika kubainisha hukumu ya mjinga katika ibada, risala katika kurejea mujtahidi kwenye fatwa yake cha Shekhe Muhammad Haadi Twaharani, na risala zingine.

Jarida huchapishwa kila baada ya muda fulani, ni maalum kwa kuandika turathi za kielimu na kukusanya maandiko ya mada za Fiqhi, Usulu, Ilmu-Rijali, Diraya na kanuni za kifiqhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: