Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya washindi wa shindano la kitamaduni, lililofanywa kufuatia kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s).
Idadi jumla ya washiriki ilifika 6793, washiriki 1293 walipata asilimia %100, wakachaguliwa washindi 10 kwa njia ya kupiga kura kimtandao, kura zimepigwa kwa ustadi na uaminifu mkubwa.
Sharti ya kupokea zawadi kwa mshindi anatakiwa ahudhurie kwenye hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s), itakayofanywa Ijumaa mwezi 3 Shabani 1447h, sawa na tarehe 23/01/2026m, katika uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) saa 12:30 jioni baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria, atatakiwa kufika katika ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi wiki mbili toka kutolewa kwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).
