Kitengo cha Dini kimehitimisha semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha semina ya awamu ya pili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Msimamizi mkuu wa semina Shekhe Ali Mujaan amesema: “Kitengo kinaendelea kufanya semina za kuwajengea uwezo watumishi wa Ataba tukufu, semina ya pili imefanywa chini ya anuani isemayo (Imamu Mussa bun Jafari –a.s-)”.

Akaongeza kuwa “Semina imedumu kwa muda wa siku kumi, wameshiriki zaidi ya watumishi 300, kulikuwa na wakufunzi bobezi kutoka hauza ya kielimu na shule ya Darul-Ilmi”.

Mujaan akabainisha kuwa “Mada za semina zimejikita katika masomo ya Fiqhi, Aqida na Qur’ani”. Akasema: “Semina imekuwa na matokeo chanya kielimu kwa washiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: