Zuwaru waliokuja katika mji wa Karbala, wamehuisha usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Shabani mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji mtukufu wa Karbala hupokea watu kutoka ndani na nje ya Iraq wanaokuja kufanya ziara katika malalo mbili takatifu, na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya imeandaa mkakati maalum wa kutoa huduma bora kwa zuwaru.







