Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya Ijumaa, imesomwa Dua Nudba iliyohudhuriwa na kundi kubwa la zuwaru.
Ibada ya usomaji wa Dua Nudba imefanywa katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Shabani, kwa ushiriki wa kundi kubwa la zuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mazingira muwafaka kwa tukio hilo la kiibada, imeandaa vitabu vya dua, sehemu maalum ya kufanyia ibada na kutoa huduma za lazima kwa zuwaru.

