Chuo kikuu cha Alkafeel kimetoa mtaala wa kitaifa uliotumiwa na vyuo vikuu vya serikali na binafsi katika mwaka 2025.
Kitivo cha famasiya, udaktari, uhandisi na teknolojia vimepata nafasi ya kwanza kwa kutimiza viwango vya wizara (IRU) kwa vyuo vikuu vya serikali na binafsi, kwa mujibu wa viwango vya Iraq katika vitengo vya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Kitivo cha udaktari wa meno kimepata nafasi ya kwanza katika viwango vya vyuo vya serikali, ufaulu huo umeonyesha mchuano mkubwa na vyuo vingine vya Iraq.
Maendeleo hayo ya kielimu yanatokana na juhudi za walimu, sambamba na kutumia mbinu za kisasa katika ufundishaji na kuweka mazingira mazuri ya usomaji yanayoendana na maendeleo ya sasa.




