Idara ya Dini tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya shindano kwa zuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kumbukizi ya mazazi ya Shaabaniyya.
Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Idara imeandaa shindano kwa zuwaru, lilikuwa na maswali mbalimbali kuhusu historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), kutambulisha utukufu wao, misimamo yao na malengo yalo matukufu”.
Akaongeza kuwa “Shindano limepata muitikio mkubwa kutoka kwa watu wa makundi tofauti, limefanywa katika mazingira tulivu.







