Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kufuatia maadhimisho ya kumbukizi ya watakatifu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani katika mji mkuu wa Baghdad.
Hafla imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Baghdad/ tawi la Zafaraniyya chini ya Majmaa, kwa kushirikiana na taasisi ya Qur’ani tukufu Sayyid Shuhadaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa waumini.
Hafla imepambwa na usomaji wa Qur’ani tukufu kutoka kwa: Sayyid Ahmadi Halo, Abdulkarim Saidi, Luay Abbasi Aljalizi, sambamba na kuimbwa beti za tenzi na mashairi kutoka kwa mwimbaji mahiri Ali Dhahabi, katika kuadhimisha tukio hili adhim.
Tukio hili ni sehemu ya harakati ya Atabatu Abbasiyya inayochangia kuimarisha mafundisho ya vizito viwili, Qur’ani na kizazi cha Mtume (a.s).





