Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imefanya hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Sajjaad (a.s) katika mji wa Waasit

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Sajjaad (a.s) katika mkoa wa Waasit.

Shekhe Abdulmuhsin Twaiy amesema: “Miongoni mwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya ya ufanyaji wa matukio ya kidini yanayohusiana na Ahlulbait (a.s), tumefanya hafla inayohusiana na kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Sajjaad (a.s) katika mtaa wa Taju-Dini mkoani Waasit”.

Akaongeza kuwa “Hafla ilikuwa na vipengele tofauti, imehudhuriwa na kundi kubwa la waumini waliokuja kuadhimisha kumbukizi ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani, mwezi ambao Maimamu kadhaa wa Ahlulbait (a.s) wamezaliwa”.

Akasisitiza kuwa “Matukio haya huleta athari kubwa katika nafsi za waumini, husaidia kuimarisha itikadi sahihi na misingi ya kufungamana na Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: