Idhaa ya Alkafeel imefanya shindano kwa mazuwaru kufuatia maadhimisho ya watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani

Idara ya Idhaa ya Alkafeel ya wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya shindano la kitamaduni kwa zuwaru, kufuatia kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.

Kiongozi wa idara Bibi Nuru-Ali amesema “Shindano limefanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lilikuwa na maswali ya kidini na kitamaduni yanayolenga kujenga uelewa na kuimarisha uhusiano na Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Idhaa huandaa mashindano katika matukio tofauti yanayohusu Ahlulbait (a.s), hiyo ni njia nzuri ya kuwasiliana na zuwaru moja kwa moja na kufikisha madhumuni ya Dini kwa namna ambayo inajenga uelewa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: