Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake katika fani ya unyenyekevu.
Semina imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa, katika mfululizo wa semina za kuwajengea uwezo watumishi wake.
Mkuu wa Maahadi Dokta Muhandi Almayali amesema, Semina ilikuwa na mada mbalimbali, kuhusu mbinu za kuonyesha unyenyekevu na namna ya kuwasiliana ndani na nje ya kazi, kwa lengo la kuimarisha utendaji kitaasisi.
Akaongeza kuwa, semina imewalenga watumishi wa idara ya mgahawa, hoteli, utoaji wa huduma mbalimbali, mapokezi na soko, chini ya mkufunzi wa kimataifa bwana Azharu Jabari.
Semina hiyo ni sehemu ya ratiba ya kuwajengea uwezo wahudumu wa Ataba tukufu na kuwafanywa waendane na malengo ya kielimu na kimalezi.





