Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mtihani wa majaribio wa nadhariya katika moja ya semina zake za maarifa ya Qur’ani katika mji wa Najafu.
Kiongozi wa idara ya hauza ya Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu, Shekhe Wasaam Sibti amesema kuwa “Semina ni sehemu ya mradi maalum wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini katika mwaka wa masomo 1447h, zinalenga kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi”.
Akaongeza kuwa “Mtihani maalum wa nadhariya umefanywa katika shule ya Daru-Ilmi, umehusisha somo ya maarifa ya Qur’ani kwa ngazi ya kwanza, kwa ushiriki wa wanafunzi 17”.
Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imefanya semina 20 katika mwaka ulioisha, wanafunzi 425 wa Dini wameshiriki kwenye semina hizo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa wa Qur’ani kwao.


