Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imeadhimisha mazazi ya miezi ya Muhammadiyya (a.s) katika mji wa Tuzikhurmatu mkoani Swalahu Dini.
Hafla imeandaliwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika kitongoji cha Tuzikhurmatu chini ya Majmaa.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Dokta Muhammad Khalili Turabi, ukafuata usomaji wa qaswida kutoka kwa Muhammad Hussein Turkumani, Muhammad Zainul-Aabidina Turkumani, Mula Hassan Asaaf, zilizo taja mapenzi na furaha kutokana na tukio hilo, sambamba na ratiba ya maswali na majibu iliyopata muitikio mkubwa kutoka kwa wahudhuriaji.
Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inalenga kuhuisha matukio yanayohusu Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kujenga uelewa wa Dini katika jamii kupitia program hizi.




