Daru-Uluum ya Nahaju-Balagha katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara wa kwanza katika hafla ya Nahaju-Balagha ya kila wiki katika Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f).
Rais wa Daru Dokta Meja Jenerali Atwiyyah amesema: “Daru imefanya muhadhara wa kwanza katika hafla ya Nahaju Balagha ya kila wiki, inahusisha kikao cha kielimu cha kusomeshana kitabu cha Nahaju Balagha na kufanyia mazigatio maana zake”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara ni sehemu ya mkakati wa Daru katika ukumbi wa haram ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), hutoa muhadhara mmoja kila wiki, hatua ya kwanza inadumu kwa muda wa mwaka mzima, inakadiriwa kuwa na mihadhara arubaini kwa mujibu wa mtaala ulioandaliwa”.


