Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinajadili maandalizi ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya kimefanya kikao cha kujadili maandalizi ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.

Rais wa kitengo Sayyid Husam Hussein amesema: “Kikao kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Afdhalu Shami pamoja na viongozi wa idara, wamejadili maandalizi ya kupokea zuwaru katika kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kikao kimeangazia mahitaji ya lazima kwa zuwaru kama vile chakula, afya, usalama na kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa ibada ya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: