Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeanza kutoa vibali kwa mawakibu zitakazoshiriki katika kuhuisha kumbukizi ya mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Kiongozi wa idara Sayyid Ali Hussein Mahadi amesema: “Kitengo kimeanza kutoa vibali kwa mawakibu zitakazoshiriki katika hafla za kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Hujjat (a.f) mwezi kumi na tano Shabani”.
Akaongeza kuwa “Vibali vinatolewa pia kwa mawakibu zinazotoka katika nchi za kiislamu zinazotaka kufanya maadhimisho katika eneo la katikati ya haram mbili takatifu”.
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hutoa ushirikiano na kurahisisha utendaji wa mawakibu kwenye matukio tofauti yanayo husu maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Karbala.


