Kitengo cha uboreshaji kinaendelea kutoa mihadhara kuhusu Nahaju-Balagha kwa watumishi wake

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea kutoa mihadhara ya kitamaduni kuhusu kitabu cha Nahaju-Balagha kwa watumishi wake.

Makamo kiongozi mkuu wa kitengo, Sayyid Haidari Ghazi amesema “Muhadhara umetolewa na Shekhe Hani Rabiy, ameeleza usia wa Imamu Ali (a.s) na barua zake tukufu, amefafanua mafundisho ya kimalezi, kimaadili na kijamii yanayopatikana, mafundisho ambayo yanasaidia kujenga uelewa wa mwanaadamu na kuimarisha maadili ya watumishi”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa katika ukumbi wa Nafidhu-Albaswirah kwenye jengo la Imamu Swadiq (a.s), lenye ofisi za vitengo vya Ataba, kwa ushiriki wa watumishi 25”.

Akabainisha kuwa “Muhadhara unalenga kujenga misingi ya kimaadili na kibinaadamu kupitia kitabu cha Nahaju-Balagha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: