Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imeadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s) katika mkoa wa Basra.
Shekhe Abduhassan Twaiy amesema: “Miongoni mwa program za Atabatu Abbasiyya ni kuadhimisha matukio ya kidini yanayofungamana na Ahlulbait (a.s), tumefanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa watakatifu ndani ya mwezi wa Shabani katika mkoa wa Basra, iliyokuwa na vipengele tofauti”.
Akaongeza kuwa “Ratiba hiyo inaathari kubwa katika nyoyo za waumini, inasaidia kutambua itikadi sahihi na kuwafungamanisha na Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.







