Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Ataba tukufu, kimekamilisha maandalizi maalum ya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.
Rais wa kitengo Sayyid Husaam Husseini amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandalizi ya kupokea zuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani chini ya makakati ulioandaliwa na sekta ya usalama na utumishi, pamoja na kuratibu harakati za zuwaru na matembezi yao”.
Akaongeza kuwa “Tumeandaa mkakati wa utoaji wa huduma, unahusisha kusafisha eneo la haram na kutandika mazulia, kuhusu ulinzi; mkakati unaanzia kwenye vituo vya ukaguzi hadi ndani ya haram na maeneo mengine”.
Akaendelea kusema “Watumishi wetu wanatumia nguvu zote kwa ajili ya kulinda usafi wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu na maeneo yanayozunguka eneo hilo”.








