Kitengo cha Dini kimeandaa zaidi ya vituo 15 vya kitablighi na kuelekeza zuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani

Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, Shekhe Swalahu Karbalai amesema, wameandaa zaidi ya vituo 15 vya kitablighi na kuelekeza zuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani.

Karbalai amesema: “Kitengo kimeweka mkakati maalum wa kiutendaji kwenye vituo vyake vilivyo ndani na nje ya haram tukufu, kwa lengo la kutoa maelekezo ya kidini, kujibu maswali ya kisheria na kuimarisha uelewa wa Dini kwa zuwaru”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa vituo 15 vya kitablighi ndani ya haram, kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili pamoja na maeneo yanayosimamiwa na wanafunzi wa hauza wanaojitolea kufanya huduma ya kujibu maswali na kutoa maelekezo ya kimaadili na kiitikadi”.

Kitengo cha Dini kupitia juhudi hiyo, kinalenga kuhudumia zuwaru wanaokuja kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: