Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza utayali wa kupokea zuwaru wa usiku wa mwezi kumi na tano Shabani.
Rais wa kitengo Sayyid Adnani Ni’mah Dhwaifu amesema “Maandalizi yalianza zaidi ya mwezi, yalihusisha uwekaji wa mikakati ya kiutendaji na kiusalama, ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa zuwaru sambamba na kuratibu matembezi yao kwenye barabara za karibu na Maqaam tukufu”.
Akaongeza kuwa “Watumishi wanafanya kila wawezalo kuandaa mahitaji ya lazima katika utoaji wa huduma, kupanga kabati za kuweka viatu, kuweka vitu, sehemu za kuswalia pamoja na kuwasiliana na kitengo cha tiba kwa ajili ya kuandaa utoaji wa huduma za dharura kwa kuweka vituo vya afya maalum kwa ajili ya kutibu zuwaru watakaopata matatizo ya kiafya”.
Akasema kuwa “Kuna mawasiliano na kituo cha waliopotelewa, ili kuweka utaratibu maalum kwa ajili ya zuwaru watakao potelewa, hususan watoto, wanawake na wazee”.
Makundi ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq yanakuja kufanya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).








