Kuzawadia washindi wa shindano la kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s)

Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi walioshinda kwenye shindano maalum la kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s).

Utoaji wa zawadi umefanywa kwenye jukwaa la hafla ikiwa ni sehemu ya ratiba ya kongamano la mishumaa awamu ya ishirini na sita, lililofanywa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s).

Kongamano limefanywa katika mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo (Mahadi ni ahadi isio ya uongo), limehudhuriwa na viongozi wa Ataba mbili tukufu, viongozi wa Dini na kundi kubwa la zuwaru.

Washindi waliokuwa na udhuru wa kushindwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, wanatakiwa kufika kwenye ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi wiki mbili kuanzia tarehe ya kutangazwa matokeo, wakiwa na nyaraka zinazowathibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: