Kazi ya kushona mabango imesimamiwa na idara ya ushonaji na udarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.
Watumishi wa kitengo wameweka mapambo ya maua na mabango yaliyoandikwa maneno ya pongezi ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na milangoni kwake, kama sehemu ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi Almuntadhwaru (a.f).
Makundi makubwa ya zuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, huja kufanya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).






