Kuweka mabango kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu kufuatia kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f)

Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mabango kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili kama ishara ya kuadhimisha kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).

Mabango yameandikwa ujumbe unaohusu tukio hilo tukufu, yametengenezwa kwa ukubwa na aina tofauti, yamewekwa sehemu mbalimbali katika uwanja wa katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kitengo kimeandaa mkakati maalum wa kuadhimisha tukio hili adhim, wenye vipengele vya kidini na kitamaduni.

Kitengo kinafanya kila liwezekanalo katika kuweka muonekano wa furaha kwenye kumbukizi za kuzaliwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) wakiwemo waliozaliwa katika mwezi mtukufu wa Shabani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: