Makundi ya zuwaru yanamiminika katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) kuja kuhuisha kumbukizi ya kuzaliwa kwake

Maqam ya Imamu Mahadi (a.s) imepokea makundi ya zuwaru wanaokuja katika mji wa Karbala kuhuisha ziara ya mwezi kumi na tano Shabani.

Makundi ya zuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq wamekuja kufanya ziara ya mwezi kumi na tano Shabani na kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinafanya kazi kubwa ya kuhudumia zuwaru watukufu, sambamba na kusimamia matembezi yao na kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa ziara na kusoma dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: