Majengo ya Shekhe Kuleini chini ya Atabatu Abbasiyya, yanatoa huduma mbalimbali kwa zuwaru wanaokuja kuhuisha usiku wa mwezi kumi na tano Shabani.
Mkuu wa majengo hayo Sayyid Hussein Tamkini Swabaru amesema “Wahudumu wa majengo wanaendelea kutoa huduma kwa zuwaru wanaokuja kuhuisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) mwezi kumi na tano Shabani, mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Huduma zilizotolewa zimejumuisha sehemu za kulala zuwaru, kugawa chakula, kutoa huduma za matibabu kwa kushirikiana na kitengo cha tiba”.
Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya wamefanya kila wawezalo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa zuwaru waliokuja kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s).













