Kwa picha.. Mazingira ya usiku wa mwezi kumi na tano Shabani mbele ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s)

Makundi ya zuwaru yamehuisha usiku wa mwezi kumi na tano Shabani mbele ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika mji wa Karbala.

Mji wa Karbala umeshuhudia makundi ya zuwaru waliokuja kuhuisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) katika usiku wa mwezi kumi na tano Shabani, kutoka ndani na nje ya taifa la Iraq.

Zuwaru wanafanya ibada ya ziara na kusoma dua katika mazingira tulivu, salama yanayowawezesha kuingia na kutoka ndani ya Maqaam tukufu bila usumbufu.

Atabatu Abbasiyya imefanya kila iwezalo karika kuhudumia zuwaru, imeandaa sehemu za kupumzika, imegawa chakula, imetoa huduma za matibabu sambamba na huduma maalum za kiibada zinazoendana na tukio hili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: