Jengo la Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya, limetoa huduma mbalimbali kwa zuwaru wa mwezi kumi na tano Shabani, wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala, ikiwa ni pamoja na ugawaji wa sahani (koshen) elfu 11 za chakula kikuu.
Mkuu wa Majmaa Sayyid Ali Mahadi Abbasi amesema “Jengo limetoa huduma kwa zuwaru waliokuja katika mji wa Karbala kuhuisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s) mbele ya malalo ya Imamu Hussein na na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), tangu usiku wa mwezi kumi na nne Shabani”,
Akaongeza kuwa “Huduma zimehusisha ugawaji wa sahani za chakula kikuu elfu 11, chakula chepesi (vitafunwa) 3600, matunda elfu 19, grasi za majii ya kunywa elfu 21 na juisi za aina mbalimbali”.
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wamefanya kila wawezalo katika utoaji wa huduma bora kwa zuwaru waliokuja kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).





