Katika kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).. kitengo cha Dini kimegawa maua na halwa kwa zuwaru

Wahudumu wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, wamegawa maua na halwa (pipi) kwa zuwaru kama ishara ya pongezi za kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Anwari Swabahi amesema: Hakika jambo hilo ni sehemu ya ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha kuhuisha matukio ya kidini na kuchangia katika kueneza furaha kwa zuwaru.

Akaongeza kuwa, kitengo kinalenga kuimarisha muonekano wa furaha katika kuadhimisha mazizi ya Imamu wa zama (a.f), sambamba na kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa zuwaru kwenye matukio tofauti ya kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: