Watumishi wa kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kusafisha barabara zote zinazoelekea Ataba tukufu baada ya kukamilika ziara ya Shaabaniyya.
Makamo rais wa kitengo Sayyid Ausi Twahir amesema: “Watumishi wa kitengo wameanza kazi ya kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, barabara ya Abbasi (a.s), Alqamiy hadi upande wa mlango wa Qibla”.
Akabainisha kuwa “Wahudumu wa kitengo wanaendelea kusafisha mji wa Karbala, kwa lengo la kudumisha usafi maeneo yote yanayozunguka Ataba tukufu na kutoa huduma bora kwa zuwaru”.





