Tamko la Atabatu Abbasiyya tukufu

Atabatu Abbasiyya tukufu inatangaza uteuzi wa Sayyid Hussein Faaiz Rasuul Hamudi Alhashimiy kuchukua nafasi ya uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, baada ya kiongozi wa zamani Sayyid Maitham Zaidi kuomba kujiuzulu, kwa lengo la kukamilisha masomo yake ya juu na kufanya kazi ndani ya Ataba tukufu.

Ataba imefafanua kuwa, Sayyid Maitham Zaidi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, ameomba rasmi kukamilisha masomo yake ya ngazi ya udaktari (digrii ya tatu), baada ya kuhitimu ngazi ya masta (digrii ya pili) miaka mitano iliyopita katika chuo cha ulinzi wa taifa jijini Baghdad (Chuo cha ulinzi wa taifa cha masomo ya kiaskari), Atabatu Abbasiyya imekubali maombi yake, na kumteua Sayyid Hussein Faaiz Alhashimiy – aliyekuwa makamo wake kuchukua nafasi hiyo, kwa lengo la kukamilisha taratibu rasmi wa kiuongozi.

Atabatu Abbasiyya inamtakia kila la kheri kijana wake mpendwa Sayyid Maitham Zaidi katika safari yake ya kielimu, inamuombea mafanikio mema katika maisha yake kielimu na kiaskari, inathamini sana juhudi kubwa alizofanya katika jihadi ya kulinda taifa la Iraq na raia wake, hususan wakati wa mapambano na magaidi wa Daesh.

Ataba tukufu inatamani arejee katika majukumu ya kijeshi baada ya kukamilisha masomo yake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ili tuendelee kunufaika na huduma zake katika kikosi cha Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu

5 Februari 2026.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: