Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) katika mkoa wa Diwaniyya, kwa kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu katika mji wa Diwaniyya kimehudhuriwa na kundi kubwa la waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Kikehusisha usomaji wa Qur’ani kwa mahadhi tofauti kutoka kwa jopo la wasomaji, usomaji wa qaswida za kimashairi zinazohusu tukio hilo.
Hafla imehitimishwa kwa ugawaji wa zawadi za tabaruku kwa washiriki, kama sehemu ya kuonyesha furaha na kuimarisha misingi ya kufungamana na Imamu Hujjat (a.f).







