Zuwaru wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala wanahuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala hupokea watu wanaokuja kutoka ndani na nje ya Iraq kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya imeandaa mkakati maalum wa kutoa huduma bora kwa zuwaru.




