Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea kutoa mihadhara kuhusu Nahaju-Balagha kwa watumishi wake.
Muhadhara umetolewa na Shekhe Haani Ribii katika ukumbi wa Nafidhu-Baswirah, ameongea kuhusu uelewa wa kifikra na kimalezi uliopo kwenye kitabu cha Nahaju-Balagha, akaangazia sekta ya kimaadili na kibinaadamu pamoja na kufafanua athari yake katika kumjenga mtu na kuimarisha mazingira ya kazi.
Mihadhara inalenga kuimarisha uelewa wa kitamaduni na kifikra kwa watumishi, sambamba na kujifunza fikra ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) katika utendaji na uajibikaji.



