Jumuiya ya Al-Ameed imefanya kikao cha robomwaka cha kwanza katika mwaka 2026 kujadili utendaji wa kiidara

Jumuiya ya Al-Ameed imefanya kikao cha robomwaka cha kwanza katika mwaka 2026 kujadili utendaji wa kiidara.

Rais wa jumuiya Dokta Sarhani Jafaat Salmaan amesema “Kikao kimejikita katika kujadili maswala ya kiidara, sambamba na kuonyesha mafanikio yake kielimu yaliyopatikana mwaka wa 2025”.

Akaongeza kuwa “Kikao hicho kimefanywa chini ya maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu nchini Iraq, yanayohimiza umuhimu wa kufanya vikao vya kiutendaji mara nne kwa mwaka, kikao hiki ni chakwanza katika ratiba ya vikao vya mwaka huu”.

Akasema kuwa: “Kikao kimehusisha ratiba ya kumpa zawadi rais mstaafu wa jumuiya hiyo Dokta Riyadhi Amidi kama sehemu ya kuthamini juhudi zake katika kuiongoza jumuiya”.

Akasisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye vikao vya kiutendaji, jambo hilo linasaidia kufikia malengo yaliyowekwa kutokana na ushiriki hai wa wajumbe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: