Katika hospitali ya Alkafeel.. mafanikio ya upasuaji wa mgonjwa mwenye tatizo la uti wa ngongo

Jopo la madaktari bingwa wa uti wa mgongo katika hospitali yarufaa Alkafeel, wamefanikiwa kufanya upasuaji wa uti wa mgongo kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka 50.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo katika hospitali ya rufaa Dokta Husaam Al-Ambaari amesema: Hakika jopo la madaktari limefanya upasuaji uliodumu kwa muda wa saa 3 na nusu, umehusisha kubadilisha pingili 14 za uti wa mgongo hadi kufikia 12 sambamba na kupitia sehemu yeto ya uti wa mgongo, ili kumpa mgonjwa uwezo wa kutembea na kumaliza tatizo la maumivu.

Akaongeza kuwa vipimo vya kina vilivyo fanywa vilionyesha uwepo wa kubana kwa mifupa ya uti wa mgongo na kuendelea kubadilika baadhi ya sehemu za uti wa mgongo sambamba kuongezeka kwa umri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: