Msafara unaongozana na watumishi wa idara, akiwemo muongozaji wa mambo ya kidini kutoka kitengo cha Dini katika Ataba tukufu, kwa lengo la kutoa maelekezo ya kidini kulingana na mahitaji ya ibada hiyo tukufu na kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi na kufikia malengo ya msafara.
Kabla ya kuanza safari imetolewa mihadhara elekezi, imefafanua ufanyaji wa ibada ya Umra, kuanzia tawafu, namna ya kuweka nia, kubainisha mambo ambayo ni haram kwa kwenye kuhirimia, swala ya tawafu na hukumu zingine zinazohusiana na ibada hiyo, pamoja na kutoa maelekezo ya kiidara, kwa lengo la kuhakikisha washiriki wanafanya Ibada ya Umra kwa usahihi.

