Kitengo cha ufundi kinaendelea na ujenzi katika barabara ya Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo cha ufundi na ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kinafanya ujenzi katika barabara ya Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara ya ujenzi wa kihandisi Mhandisi Muhammad Abdu-Nabi amesema “Hakika mafundi wanaendelea na ujenzi katika barabara ya Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ujenzi huo unahusisha uwekaji wa zege kwenye eneo lenye ukubwa wa mita 900 kaada ya kusawazishwa sehemu hiyo na kitengo cha miradi ya kihandisi katika Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa, Kazi imefanywa kwa kutimiza vigezo vyote vya kihandisi kwa ufanisi mkubwa, bila kuzuwia harakati za zuwaru na imependezesha muonekano wa barabara.

Kitengo kinalenga kuboresha utoaji wa huduma katika eneo lote linalozunguka Atabatu Abbasiyya na vitengo vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: