Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amepokea ugeni kutoka shirika la (Sitifarma) nchini Pakistani linalojihusisha na dawa.
Muheshimiwa amesikiliza maelezo kutoka kwa katibu mtendaji wa shirika Sayyid Ridhwani Ahmadi, kuhusu kazi za shirika katika sekta ya utengenezaji wa dawa.
Makamo katibu mkuu katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema: Hakika Atabatu Abbasiyya inajenga ushirikiano na mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya dawa na vifaa-tiba, kwa lengo la kuwa na vifaa-tiba bora zaidi kulingana na mahitaji ya jamii.
Akaongeza kuwa, juhudi za Ataba tukufu zinalenga kuimarisha soko la dawa kitaifa, na kuchangia uingizaji wa dawa bora zaidi kimataifa, jambo linalosaidia upatikanaji wa dawa na uhakika wa utoaji wa matibabu kwa wananchi.
Katibu mtendaji wa shirika amesema: Hakika kukutana na muheshimiwa Sayyid Swafi tumepata nafasi ya kujadili ushirikiano baina yetu na Ataba tukufu.
Akaongeza kuwa, Ugeni umeangazia miradi ya utengenezaji wa dawa, akasema kuwa ziara ilikuwa nzuri, kunajitihada za kufungua sekta mpya za ushirikiano.



